- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KUONGEZEKA KWA MATUMIZI YA MTANDAO KUMESABABISHA VIASHIRIA VYA KUHATARISHA USIRI WA TAARIFA.
DODOMA: Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dk. Maria Sasabo amesema kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya Mtandao Nchini zimetokea Changamoto za viashiria vya matishio ya kuhatarisha usalama na usiri wa Taarifa.
Dk Sasabo ameyasema hayo wakati akifungua mafunzoya Usalama Mtandaoni (Cyber Security) yaliyoshirikisha Taasisi Mbalimbali za Kiserikali yaliyofanyika leo Jijini Dodoma.
‘’Kwa kuwa utandawazi haujali Mipaka ya Nchi inabidi tuwe makini na Tujipange kukabiria na Viashiria au Matukio hatarishi endapo yatatokea kwa haraka nimeambiwa kuwa hili ndio lengo kuu la mafunzo ambayo yatatolewa kwa kipindi cha Wiki nzima,’’ amesema Dk huyo.
Ameendelea kwa kusema mafunzo hayo yatasimamia na kuzingatia kwakutoa namna ya utambuzi wa hatua za kuchukua lakini pia kujenga ushirikiano baina yao , Taasisi moja na nyingine na namna ya kukabiliana na changmoto kwa kuweka kinga katika mifumo na kutoa elimu kwa watumiaji Mitandao.
Amesisitiza kuwa mafunzo yatakayotolewa na mamlaka ya Mawasilano Tanzania kwa Kushirikiana na Serikali Mtandao yatasaidia katika kujenga maadili katika kulinda na kutunza taarifa Muhimu, Kukinga Taarifa zisitumike bila idhini, kulinda Taswira na kupunguza gharama za Matumizi au hasara zinazoweza kutokea kutoka na matumizi yasiyo salama ya Mtandao.
‘’Napenda Niwathibitishie kuwa TCRA pamoja Serikali Mtandao wamejipanga na wapo tayari kuendelea kutoa huduma za Elimu kuhusu kinga, thathimini na namna ya kufanya ‘Assessment’kupima uhimilivuwa mifumo , kupendekeza teknolojia sahili na nyinginezopasipo gharama kwa Taasisi, kwahiyo natoa Wito kwenu Mkawe mkawe mabalozi wa kufanya Tathimini hizo, kulinda Mifumo na kutoa Elimukatika Taasisi,’’amesema Mhandisi Sasabo.
Mbali na hayo amesema Serikali imeweka mdhibiti wa sekta ya mawasilano ambaye ni mamlaka ya mawasiliano Tanzania ,wakala wa Serikali mtandao ambaye anasimamia na kuhimiza matumizi ya Tehama serikalini TEHAMA Sheria ya miamala ya kielekroniki na posta maarufu kama epoka,sheria ya miamala ya kielektroniki,sheria ya makosa ya mtandao na sheria ya mfuko wa sekta ya mawasiliano kwa wote na vyote hivi vitahusika kuwa nataasisi pamoja na kuwa na kitengo cha kuhusisha usalama kwa njia ya mtandao itakayo ratibu matukio viashiria hatarishi katika usalama wa viashiria vya Kimtandao kitaifa.
Mkrugenzi wa Mawasiliano kanda ya kati Antonio Manyanda amesema kuwa mafunzo hayo yametolewa kwa maafisa Tehama wa taasisi zote za Serikali ili kuwapa ufahamu kuhusiana na makosa ya Mtandaoni namana ya kutambua mambo ya usalama ya mtandao ili taarifa mbalimbali za umma zisije zikakamatwa na kudukuliwa na watu ambao hawahusiki.
Pia amesema kuwa taasisi hizo zipo tayari katika kila taasisi ya umma kwa ajili ya kuangalia usalama zaidi endapo hatari yeyote inaweza kutokea katika shambulio la kimtandao serikalini na kueleza kuwa mpaka sasa hali ya kimtandao hapa nchini ipo salama .