Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 11:23 am

NEWS: KUNCHELA ALIA NA UWEZESHWAJI WA VIJANA

Dodoma: MBUNGE wa viti Maalum, Rodha Kunchela (Chadema) ameibana serikali na kutaka ieleze ina mikakati gani ya kusaidia vijana ili waweze kupata ajira pamoja na kuwapa mazingira wezeshi ya kujikwamua kiuchumi.

Kunchela aliihoji serikali jana bungeni wakati aliuliza swali la msingi kwa lengo ya kutaka kujua nini mikakati ya serikali kuwawezesha vijana katika kuwakwamua katika umasikini.

“Ipo changamto kubwa ya ukosefu wa ajira kwa vijana wa mkoa wa Katav, ikichangiwa na miundombinu mibovu inayosababisha wawekezaji kushindwa kuwekeza.

“Je serikali ina mikakati gani ya kusaidia vijana hao wapate ajra na kuwa na mazingira wezeshi ya kujikwamua kiuchumi” amehoji.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Selemani Jafo, alisema,serikali ina mikakati ya kuhakikisha vijana wa mkoa wa katavi wanawezeshwa katika kupata mitaji na kuandariwa mazingira rafiki.

Amesema serikali inazielekeza Mamlaka za serikali za Mitaa kuzingatia masuala ya ukuzaji wa ajira katika mipango ya maendeleo hususani kutambua na kubaini mahitaji ya nguvu kazi katika maeneo husika.

Amesema pia kuna kila sababu ya kutenga na kuendeleza maeneo ya uzalishaji biashara kwa vijana,ili kuwezesha nguvu kazi kuwa na ujuzi wa kujiajiri, kuwezesha upatikanaji wa mitaji na vitendea kazi kwa makundi ya vijana,kukuza soko la bidhaa na huduma za wajasiliamali hasa vijana.

Serikali inatekeleza program ya miaka mitano ya kukuza ujuzi inayolenga kuwezesha vijana 4,419,074 kupata ujuzi wa kuajiliwa au kujiajiri katika sekta mbalimbali.

katika mwaka wa fedha 2016/7 vijana 1,469 wamepatiwa mafunzo ya ushonaji wa nguo kupitia viwanda vya mavazi .