- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ''KUMEKUWA NA ONGEZEKO LA WATOTO WANAUJIUNGA NA ELIMU YA AWALI ''NAIBU WAZIRI WAITARA.
MWAZA: Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mwita Mwikwabe Waitara amesema tangu kuanzishwa kwa sera ya mafunzo ya elimu ya mwaka 2014, kumekuwa na ongezeko la watoto wanaojiunga na elimu ya awali kutoka milioni moja mwaka 2015 hadi watoto milioni moja na nusu mwaka 2016.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa madarasa manne kati ya madarasa 30 yanayojengwa kwa ushirikiano baina ya serikali na shirika lisilo la kiserikali la children in crossfire katika Halmashauri za Misungwi na Ukerewe wilaya ya MisungwiMkoani Mwanza Waitara ameziagiza halmashauri kuhakikisha kuwa kila inapojenga shule za msingi pia inapaswa kuweka bajeti kwa ajili ya darasa la awali.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa shirika la kimataifa la Children in Crossfire bwana Craig Ferla amesema kuwa shirika hilo katika kipindi cha miaka minne ijayo limepanga kutumia shilingi milioni 700 kwa ajili ya kujenga madarasa 100 ya aina hiyo katika mikoa ya Mwanza, Morogoro na Dodoma.
Naye Mratibu wa mafunzo ya elimu ya awali kutoka shirika hilo Davis Gisuka amesema kuwa mbali na kujenga madarasa hayo ambayo yanaongea na kucheka pia wanatoa mafunzo kwa walimu wa shule za awali za serikali ili waweze kumudu kuwapatia elimu watoto wanaowafundisha kupitia mbinu mbalimbali za mafunzo ikiwemo matumizi ya zana rahisi za kufundishia zinazotengenezwa na walimu hao katika shule zao.