- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KUBENEA SIRI ZITO NA BAWACHA
DAR ES SALAAM: MBUNGE wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea, amewataka viongozi wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), jimbo la Ubungo, kukitetea na kulinda chama chao kwa gharama yeyote ile kwa kuwa wanawake hao, ndio nguzo muhimu ya chama hicho,
Ametoa kauli hiyo leo jioni katika ofisi za Chadema kata ya Mabibo, jijini Dar es Salaam.
Katika kikao hiko cha ndani mbunge huyo aliwasihi wanawake kukilinda chama chao, kulinda mafanikio yaliyopatikana hasa katika uchaguzi mkuu uliopita na kukitetea ili kkuhakikisha kinaingia Ikulu mwaka 2020.
Amesema,” mafanikio haya tulioyapata siyo haba, ingawa tulistahili kupata makubwa zaidi. Naomba tuyalinde na kuhakikisha tunapata mafanikio makubwa zaidi.”
Akizungumza kwa hisia kali, Kubenea amesema, wanawake ni watu muhimu katika ukuaji wa chama na udumishaji wa demokrasia.
Hivyo basi, aliwataka kuendelea na moyo huo kwa ustawi mpana wa chama hicho na taifa.
“Wanawake ni watu muhimu sana hasa katika ukuaji wa demokrasia ya nchi hii. Nawaombamzidi kuendelea kuwa na mshikamano huo huo na kuwa wamoja,” amesema Kubenea.
Kwa mujibu wa Kubenea, Chadema kimekuwa kwa kasi ndani ya miaka miwili iliyopita, lakini kasi hiyo inakabiliwa na changamoto ya kuogopwa na Chama Cha Mapinduzi na hivyo, kuvitumia vyombo vya dola kukiandama.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa Kinondoni, Suzan Lymo na Mwenyekiti wa Bawacha mkoa wa Kinondoni, Magreth Mugyabuso.
Viongozi hao kwa pamoja waliahidi kutoa ushirikiano kwa mbunge na wanawake wote ili kuhakikisha chama hicho kinaendelea kuwa imara.
Kubenea yupo katika ziara ya kichama ya siku 14 kwa lengo la kuimarisha chama.