Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 9:39 am

NEWS: KUBENEA ATINGA MAHAKAMANI

DODOMA: MBUNGE wa Ubungo,SAED KUBENEA amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Dodoma kwa kosa la kumshambulia Mbunge wa Viti Maalum JULIANA SHONZA.

Akimsomea shitaka hilo leo Mbele ya Mahakama hiyo ,Mwanasheria wa Serikali BAETRICE NSANA amesema kuwa mshitakiwa KUBENEA anakabiliwa na kosa la shambulio kinyume cha Sheria kifungu namba 240 cha sheria ya makosa ya jinai sura ya 16 kilichofanyiwa marejeo mwaka 2002.

BI.NSANA amebainisha kuwa mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo Juali 3 mwaka huu katika eneo la Bunge Mjini Dodoma.

Kwa upande wake mshitakiwa SAED KUBENEA alipoulizwa na Hakimu JAMES KARAYEMAHA kuhusiana na kutenda kosa hilo,alikana shitaka.

Hakimu KARAYEMAHA amesema kuwa dhamana ipo wazi ambapo anatakiwa mdhamini wa kudumu na kiasi cha Sh Milioni moja ambapo mshitakiwa alikamilisha vigezo hivyo na yupo nje kwa dhamana.

Hata hivyo upelelezi wa Kesi hiyo namba 116 haujakamilikana kesi imeahirishwa hadi Julai26 mwaka huu.

Kesi hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa,FREEMAN MBOWE.

Akiongea nje ya Mahakama hiyo,Mwenyekiti huyo ameonyeshwa kusikitishwa na kitendo hicho kwani ni jambo la kufedhehesha sana kwao kutokana na Wabunge wake namna wanavyo jiheshimu.

Naye Wakili wa kujitegemea FRED KALONGA na JAMES OLE MILLYA ambao wana mtetea KUBENEA wamesema kuwa wana imani na Mahakama kwani ni chombo cha kutenda haki hivyo haki itapatikana.