Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 3:19 am

NEWS: KUBENEA ACHARUKA BUNGENI

DODOMA: MBUNGE wa Ubungo Saed Kubenea (Chadema) amelitaka Bunge kuacha kuwazuia wabunge kuwajadili viongozi wenye migongano ya maslahi katika mikataba ya hovyo iliyoliingiza taifa hili kwenye hasara.

Kubenea alisema hayo bungeni jana alipokuwa akijadili Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2017/2018 na kusema lazima wajadiliwe na washitakiwe kwa kulisababishia hasara taifa hili.

“Mgongano wa maslahi upo kwa viongozi wetu wakubwa, Balozi Ami Mpungo alikuwa wetu wa Balozi Afrika Kusini akawa dalali wa makaburu walionunua NBC, waliochimba Tanzanite. Baada ya kustaafu akawa mmoja wa wamiliki wa Kampuni ya madini ya Afgem.

Daniel Yona akiwa Waziri wa Nishati na Madini alipeleka dokezo kwenye Baraza la Mawaziri la kuuza Kiwira. Kiwira ikauzwa akaanzisha kampuni ya Tanpower akaingia ubia wa kampuni nyingine ya Anben Limited, wakauziana Kiwira na ilivyokwenda mnaijua.

“Leo tukaa hapa tunazungumza kana kwamba hayo mambo hayapo eti tusiwajadili watu waliohusika kuingiza nchi hii kwenye migogoro ya kifisadi.

“Hii mikataba yote ni ya CCM na serikali yao wasichukue kesi isiyotuhusu wakatutupia sisi, hilo ni dudu lao wameliamsha… wamalizane nalo wenyewe.

“Eti tumeibiwa katika rasilimali zetu na watu waliokuja kuwekeza, mikataba iliyofungwa imefungwa kwa sheria zilizopo, waliofunga mikataba hiyo mmoja wao amesema hakamatiki.

“Anasema mikataba hiyo imefungwa baada ya kikao cha Baraza la Mawaziri kukutana na kuwepo ‘minutes’ za vikao hivyo hatuwezi kusema tumeibiwa wakati tumeruhusu mali yetu wenyewe.

“Ningeelewa tungesema mikataba tuliyoifunga ya kinyonyaji wizi, mtu anaondoka kwenye nchi yako anagonga stempu, analipa ushuru anakulipa hela yako anaondoka unasema amekuibia.

“Kuonesha kwamba hakuna mwizi Rais Magufuli alikaa na mwizi wakazungumza, milango ya Ikulu ilifunguliwa mwizi akaingia, rais akakaa na mwizi. Nilitegemea rais angeenda kumweka ndani,” alisema Kubenea kabla ya Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan ‘Zungu’ kumzuia kutaja neno mwizi bungeni.

Akiendelea kuchangia, mbunge huyo ambaye kitaaluma ni mwanahabari alimtaja Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa kuwa miongoni mwa viongozi waliolisababishia hasara kubwa taifa hili.

“Mwaka 2011 kuna mwaliko kutoka China wanaalikwa Mwambalaswa mwenye passport namba AB002021 iliyotolewa Januari,2006 katika mwaliko huu anakwenda na William Mhando aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco wengine.

“Wanasema wanakwenda kufunga mkataba kati ya Tanesco na kamapuni ya China ya Power East Afrika Limited ambayo ni yake anasafiri kwa pesa ya Tanzania, analipwa posho ya Tanesco kwenda kufunga mkataba na kampuni yake halafu anakuja hapa anasema lile lilikuwa wazo.

“Hii hapa taarifa ya NBC inasema mradi wa umeme wa upepo wa Singida PT 33162 umeanza 2010 mradi unatekelezwa na Power Pool East Afrika Limited ya kwa mwaka 2010 Bashiru Mrindoko anatoa barua hii ya kuipa kazi kampuni ya kina Mwambalaswa,

“Mwaka 2010 Sitta (aliyekuwa Spika wa Bunge) anafunga majdala wa Richmond bungeni kwa ubabe tu. Mwaka 2011 Mwambalaswa anakuwa mwenyekiti wa Kamati yaBunge ya Nishati na Madini na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco ndio maana tunasema mgongano wa maslahi.

“Halafu hapa mnasema mnafukua makaburi fukueni haya, kuna mgongano wa maslahi mkubwa, ninaorodha ndefu ya viongozi wa serikali hii ambao mikataba iliyofungwa wanamaslahi nayo.

“Kuna mtu amesimama hapa asubuhi anasema anampongeza Rais Magufuli namuomba akaangalie fedha iliyotumika kulima IPTL mwaka 2010 kuelekea kipindi cha uchaguzi mkuu sh. bilioni 46 kulipia mafuta ya IPTL kwa mwezi walilipa sh. bilioni 15 Ngeleja akiwa Waziri wa Nishati na Madini na ndiye aliyesaini hiyo,” alisema na kuviomba vyombo vya ulinzi na usalama viwachunguze watu hao.

Awali mbunge huyo alisema hakuna mtu anayepinga juhudi za Rais Magufuli za kuokoa rasilimali za nchi hii zilizokuwa zitafunwa kama shamba la bibi