Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 12:35 pm

NEWS: KOREA YAFANIKIWA KUTENGENEZA BOMU KALI ZAIDI DUNIANI LA HAIDROGENI

Pyongyang: Korea kaskazini imefaniliwa leo Jumapili (03.09.2017) kutengeneza bomu la aina haidrojeni lenye "uwezo mkubwa wa maangamizi" Ripoti kutoka Korea Kaskazini imetangaza kwamba imefanikiwa kufanya majaribio ya bomu la haidrojeni - aina ya bomu la nyuklia, Ripoti hiyo iliyotolewa na shirika rasmi la bahari la Korea kaskazini KCNA inakuja wakati kuna hali ya juu ya wasi wasi katika eneo hilo kufuatia majaribio mawili ya makombora yanayoweza kuvuka bara moja hadi jingine mwezi Julai ambayo yana uwezo wa kuruka kiasi ya kilometa 10,000 , na kuyaweka maeneo mengi ya Marekani kuweza kufikika.

Chini ya kiongozi wa kizazi cha tatu Kim Jong Un , Korea kaskazini imekuwa ikiwania kutafuta silaha za kinyuklia ndogo na nyepesi kuweza kuwekwa katika kombora la masafa marefu, bila kuathiri uwezo wake wa kuruka na kulifanya kuwa na uwezo wa kuhimili kuingia katika anga la dunia.

mbayo inafanya mipango yake ya makombora na nyuklia kwa kukaidi maazimio na vikwazo vya baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa , "hivi karibuni ilifanikiwa" kuitengeneza bomu la hali ya juu kabisa la haidrojeni ambalo linaweza kuwekwa katika kombora la masafa marefu la ICBM, limesema shirika hilo la habari la KCNA.

Bomu hilo la haidrojeni , uwezo wake wa kuripuka ambao unaweza kurekebishwa kutoka mamia ya kilotani na kuwa maelfu ya kilotani, ni bomu la nyuklia lenye uwezo wa aina mbali mbali na uwezo mkubwa wa maangamizi ambalo linaweza kuripuriwa hata katika kima kirefu kwa kutumia vifaa vyenye nguvu kubwa ya shambulizi vya EMP , (electromagnetic pulse) kwa mujibu wa lengo lake la kimkakati, shirika la habari la KCNA limesema.