November 24, 2024, 2:49 pm
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KOREA YA KASKAZINI YAFYATUA KOMBORA LA MASAFA MAREFU
Pyongyang: Nchi ya Korea ya kaskazini leo hatimaye imefanikiwa kufanya jaribio la kombora la masafa marefu, kombora hilo lilikwenda umbali wa kilometa 7,000 kabla ya kuanguka mpakani kati ya Korea kaskazini na Japan.
Baada ya jaribio hilo Marekani inataka vikwazo zaidi viongezewe katika taifa hilo huku Ikulu hiyo ya White House ikisema kuwa, Pyongyang imeachwa kwa muda mrefu katika kutekeleza majaribio yake hayo ya makombora.
Rais mpya wa Korea Kusini Moon Jae-in, amelaani kitendo hicho cha Korea Kaskazini, cha kufanya majaribio zaidi ya zana zake za mafasa marefu, akilitaja kama kitendo cha uchochezi dhidi yake.