- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KOREA KASKAZINI YAWEKEWA VIKWAZO VIPYA NA UMOJA WA MATAIFA
New York City: Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha vikwazo vipya dhidi ya Korea Kaskazini siku ya Jumatatu, Septemba 11. Vikwazo hivyo ambavyo ni kama adhabu ya kufanyia majaribio zana zake za nuklia, vinalenga kuhujumu uwezo wa Pyongyang kufadhili na kutoa kawi kwa mpango wake wa nuklya. Reuters
Maamuzi hayo ya baraza la usalama la umoja wa mataifa yaliungwa mkono kwa wingi wa kura baada ya Marekani kuondoa mpango wake wa kutaka uungwaji mkono kutoka Urusi na China
Miongoni mwa vikwazo hivyo ni pamoja na kupiga marufuku mauzo ya nguo kutoka Korea Kaskazini na kupunguza kiwango cha mafuta na gesi. Kwa masharti haya mapya, wanadiplomasia wana matumaini ya kuzuia 90% ya mauzo ya nje ya Korea Kaskazini na kupunguza mauzo yake ya mafuta kwa 30%. Vikwazo hivyo vilichukuliwa kwa pendekezo la Marekani, lakini si kama utawala wa Trump ulivyotarajia
Kwa upande wa Marekani, Uingereza, Ufaransa au Italia, azimio lililopitishwa siku ya Jumatatu ni "vikali" na vyenye "uwiano". Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley, alikaribisha msimamo wa China na Urusi kwa kuunga mkono vikwazi hivyo na kutuma ujumbe wa umoja. "Leo tunasema kwamba ulimwengu hautakubali Korea Kaskazini kuendelea na zana zake za nyuklia. Na leo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linasema kuwa kama Korea Kaskazini haitoachana na mpango wake wa nyuklia, tutachukua hatu sis wenyewe, " amesema Balozi Nikki Haley.