- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KOREA KASKAZINI YARUSHA MAKOMBORA MENGINE MAWILI
Jeshi la Korea Kusini limesema kuwa Majirani zao Korea Kaskazini wamerusha vifaa viwili vya moto ambavyo havikutambuliwa mara moja na kuanguka katika baharini, na ni masaa machache baada ya nchi hiyo kutoa pendekezo la kuanzisha mazungumzo ya kidiplomasia ya kinyuklia na Marekani lakini ikaonya kuwa shughuli zake na Marekani huenda zikafikia kikomo bila ya mapendekezo mapya.
Hatua hiyo ya Korea Kaskazini na matakwa ya mapendekezo mapya yamelenga kuishinikiza Marekani kufikia makubaliano wakati mazungumzo kati yao yatakaporejelewa tena. Inaaminika kuwa Korea Kaskazini inaitaka Marekani kuipa hakikisho la usalama na afueni ya vikwazo vinavyoongozwa na Marekani kwa taifa hilo kupunguza hatua zake za kinyuklia. Jeshi la Korea Kusini limesema litafuatilia uwezekano wa majaribio zaidi lakini halikutoa habari zaidi kuhusu vifaa vilivyorushwa na Korea Kaskazini.