November 26, 2024, 10:51 am
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KOREA KASKAZINI YARUSHA KOMBORA KUBWA KWENYE ANGA YA JAPANI
pyongyang: Korea Kaskazini imerusha kombora kubwa kuelekea bahari ya Japan, Kombora hilo lilipita kwenye anga ya kaskazini mwa Japan, kwa mujibu wa serikali ya Japani, taarifa iliyothibitishwa na Pentagon.
"Kombora lisilojulikana" lilirushwa kutoka Sunan karibu na Pyongyang saa 5:57 saa za Korea Kaskazini (sawa na saa 20:57 siku ya Jumatatu, usiku saa za kimataifa), kwa mujibu wa uongozi wa jeshi la Korea Kusini. "Korea Kusini na Marekani wanatathmini kwa pamoja hali hiyo," uongozi wa jeshi la Korea Kusini umeongeza. Kombora lililorushwa na Korea Kaskazini inaonekana kuwa lilipita kwenye anga ya Japan, kwa mujibu wa shirika la habari la Kyodo. Kwa mujibu wa NHK, kombora hilio lilipasuka vipande vitatu na lilianguka katika pwani ya kisiwa cha Hokkaido.Mfumo wa onyo wa mamlaka uliwashauri wakazi wa eneo hilo kuchukua tahadhari, lakini kwa mujibu wa kituo cha habari cha serikali ya Japan, hakuna hasara iliyotokea. Msemaji wa Waziri Mkuu, Yoshihide Suga, amesema kuwa kombora hilo ni "tishio kubwa kwa usalama" wa Japan.Tukio hilo limechochea tahadhari ya hatari ambayo watu walielekezwa kujificha katika maeneo yaliyo chini ya ardhi ama kwenye majengo yaliyo imara.
Hakuna juhudi zilizofanywa na Japan kulitengua kombora hilo lakini ilitoa onyo la kiusalama ikiwaambia raia wake katika eneo la Hokkaido kujificha chini ya majumba yaliojengwa ardhini.Wakati huo huo Bwana Abe alisema kuwa amezungumza na rais wa Marekani Donald Trump na kwamba wote wamekubaliana kuiongezea shinikizo Korea Kaskazini.