- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KOREA KASKAZINI YAHARIBU HALI YA G7 YAFYATUA MAKOMBORA 2
Taifa la Korea Kaskazini limefyatua makombora mawili ya masafa mafupi baharini yenye ubora wa hali ya juu, Taarifa hii ni kulingana na jeshi la Korea Kusini.
Hatua hiyo ya Korea Kaskazini kufyatua makombora hayo yametafsiriwa kuwa ni ujumbe kwa wajumbe wa mkutano wa nchini Tajiri zaidi Duniani maarufu kama G 7 Unaofanyika nchini Ufaransa.
Kwajumla sasa Jaribio hilo linakuwa ni la saba kutekelezwa tangu Korea Kaskazini ilipomaliza mpango wake wa miezi 17 wa kusitisha majaribio yoyote ya silaha zake.
Jaribio hilo lilisimamiwa na rais wa taifa hilo Kim Jong Un kulingana na chombo cha habari cha taifa hilo KCNA. Chombo hicho kilisema kwamba lilikuwa jaribio la kombora kubwa ambalo ilisema liliundwa hivi karibuni.
Kim Jong un alilitaja kombora hilo kuwa silaha nzuri huku akilishukuru kundi la watalaam waliounda makombra hayo, KCNA ilisema.
Maafisa wa kijeshi wanasema kwamba makombora hayo yalirushwa saa kumi na mbili na dakika arobaini na tano na saa moja na dakika mbili muda wa Korea Kaskazini kutoka mji wa mashariki wa Sondok kusini mwa mkoa wa Hamgyong.
Wanasema kwamba makombora hayo yaliruka umbali wa kilomita 380 na urefu wa kilomita 97 kabla ya kuanguka katika bahari ya Japan, pia ikijulikana kama bahari ya mashariki.
''Jeshi letu linachunguza hali ilivyo iwapo majaribio zaidi yatafanyika huku tukujiandaa'' , alisema mkuu wa jeshi wa Korea Kusini.
Waziri wa ulinzi wa Japan , Takeshi Iwaya alihibitisha kombora hilo halikuanguka katika maji ya Japan lakini akataja kuwa ni ukiukaji wa wazi wa maazimio ya Umoja wa Mataifa.