Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 3:35 pm

NEWS: KOREA KASKAZINI YAFYATUA TENA MAKOMBORA MAWILI

Korea Kaskazini imefanya uzinduzi wa majaribio ya makombora mapya mawili ya masafa mafupi Alhamisi jana, Mei 9, alasiri.

Makombora hayo yaliyorushwa kuelekea mashariki mwa nchi, moja lilikwenda umbali wa kilomita 420 na nyingine kilomita 270 yakiwa hewani,kwenye anga ya Korea Kaskazini, kabla ya kuanguka katika Bahari ya Japan.


Hatua hii inakuja siku tano tu baada ya mfululizo wa vifaa vya kulipuka kurushwa Jumamosi, Mei 4, kwenye Bahari ya Japani.


Utawala wa Kim Jong-un unaonekana kuwa unajaribu kuweka shinikizo kwa Marekani na Korea Kusini, wakati mazungumzo ya nyuklia yamesimama. Makombora haya mawili ya masafa mafupi yamerushwa kutoka kambi ya Sino-ri, kilomita 77 kaskazini magharibi mwa Pyongyang, jeshi la Korea Kusini limesema.

Makombora haya yamerushwa wakati mjumbe maalum wa masuala ya nyuklia wa Marekani, Stephen Biegun, amewasili Alhamisi hii jijini Seoul kwa mazungumzo. "Korea Kaskazini imetaka kuonyesha Marekani kwamba suala haliko upande wao," mchambuzi Andrey Lankov kutoka Seoul amesema.



Ameongeza kuwa utawala "utaendelea kukumbusha kuwa ikiwa mkataba kuhusu vikwazo hautopatikana, basi inaweza kusababisha hali ya sintofahamu katika ukanda huo".



Urushaji huo wa makombora unakuja wakati Korea Kusini ina mpango wa kutoa msaada wa kibinadamu kwa raia wa Korea Kaskazini, wanaokabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula