- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KOREA KASKAZINI YAENDELEA KUITISHA MAREKANI KIVITA
Pyongyang: Korea Kaskazini imeedelea kutoa matamko makali dhidi ya Marekani hasa pale ambapo Marekani inapotoa tamko la kusitishwa kwa majaribio ya kurusha makombora kwa Korea kaskazini, jana Afisa wa juu nchini koria amehojiwa na chombo cha habari cha BBC mjini Pyongyang, kuwa itaendelea kufanya majaribio ya makombora yake,ingawa jamii ya kimataifa imekuwa ikikemea majaribio hayo.
Hapa ni makombora yakisongezwa kuelekea Upande wa korea ya kusini yapo majeshi ya marekeni
Makamu waziri wa masuala ya kigeni Han Song-ryolJohn Sudworth. alisema kuwa ''Tutatekeleza majaribio zaidi katika kipindi cha kila juma,kila mwezi na kila mwaka,"
Awali, Makamu wa rais wa Marekani, Mike Pence aliionya Korea kutoijaribu Marekani, akisema kuwa muda wa kuivumilia nchi hiyo kwa miaka mingi umekwisha.
Hizi ndizo zana za kinuklia za korea kaskazini
Bwana Pence aliwasili mjini Seoul nchini Korea Kusini mwishoni mwa juma lililopita baada ya Kombora la Korea kaskazini kushindwa kupaa.
Hali ya wasiwasi imekuwa ikiongezeka katika eneo la Peninsula, wakati huu kukiwa na hali ya kushambuliana kwa maneno baina ya Korea kaskazini na Marekani.
Bw Han alisema kuwa: ''Ikiwa Marekani inapanga kutekeleza shambulio la kijeshi dhidi yetu tutachukua hatua ya kupambana kwa shambulio la Nuklia kwa mbinu zetu na mtindo wetu.