Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 6:33 pm

NEWS: KOREA KASKAZINI " TUNAWEZA KUISAMBARATISHA MAREKANI KOKOTE PALE"

Pyongyang: Nchi ya korea kaskazini kupitia Rais wao Kim Jong-un wamesema kuwa kwa sasa wanauwezo wa kuipiga marekani wakiwa kwenye Himaya yao kutokana na kuwa namakombora yanayoweza kusafiri hadi nchini marekani, imesema kuwa imefanikiwa kufanyia jaribio kombora lake la masafa marefu ICBM, Kim alisema kuwa jaribio hilo lilibaini kwamba marekani yote ipo katik rada yao na sasa inaweza kushambuliwa wakati wowote kama nchi itaamua.

Jaribio la kombora hilo linajiri wiki tatu baada ya jaribio la kombora la kwanza la masafa marefu la Korea Kaskazini.

Rais wa Marekani Donald Trump amelitaja jaribio hilo kuwa la kijinga na kitendo cha hatari kilichotekelezwa na utawala wa Korea Kaskazini .

China pia imeshutumu jaribio hilo huku ikitaka pandfe husika zilizo na waiwasi kujizuia ili kutoendeleza wasiwasi zaidi.

Ikithibtisha kurushwa kwa kombora hilo, Korea Ksakzini ilisema kuwa kombora hilo la masafa marefu liliruika kwa dakika 47 na kufika urefu wa kilomita 3,724.

Imesema kuwa jaribio hilo lilifanikiwa kujaribu uwezo wa kombora hilo kuingia.

Kiongozi huyo pia alisema kuwa jaribio hilo lilithibitisha kwamba Korea Kaskazini sasa ina uwezo wa kushambulia ardhi yoyote ya Marekani kulingana na chombo cha habari cha Yonhap.

Taarifa hiyo ilisema kuwa kombora hilo ni Hwasong 14 kombora sawa na lile lililojaribiwa Julai 3.