Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 11:16 pm

NEWS: KOREA KASKAZINI KUFUTA KURUDIA MKUTANO NA MAREKANI

Viongozi wa Korea Kaskazini wanaushuku umuhimu wa kuendelezwa mazungumzo kuhusu mradi wa nuklea wa Pyongyang na Marekani hii ni Baada ya kushindwa mkutano wa kilele kati ya Kim Jong Un na rais wa Marekani Donald Trump, wiki mbili zilizopita nchini Vietnam.

Image result for kim jong un

Korea ya kaskazini haina azma ya kuridhia masharti ya Marekani, amenukuliwa naibu waziri wa mambo ya nchi za nje Choe Son Hui akisema.

Shirika la habari la Urusi-Tass lililoripoti habari hizo linasema kiongozi wa Korea ya Kaskazini Kim Jong Un anapanga kutoa taarifa hivi karibuni kuhusu muongozo mpya. Pande hizo mbili, zimeshindwa kukubaliana wakati wa mazungumzo ya Hanoi kuhusu suala muhimu ya kusitishwa mradi wa nuklea wa Korea ya Kaskazini ili iweze kuondolewa vikwazo na Marekani.