- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KOREA KASKAZINI IMEFANYA MAJARIBIO SILAHA ZAKE MPYA ZENYE NGUVU
Taifa la Korea Kaskazini limesema limefanyia majaribio silaha zake mpya, iliyozieleza kuwa ni silaha ya mwongozo iliyo na nguvu kuliko, likiwa ni jaribu la kwanza baada ya mazungumzo kati ya kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un na rais wa Marekani Donald Trump kumalizika bila ya mwafaka wowote miezi kadhaa iliyopita.
Ripoti ya kina haijatolewa kuhusu jaribio hili. Wadadisi wa mambo wanaona kuwa huenda hii sio ishara kuwa Korea Kaskazini inataka kurejelea majaribio ya silaha zake za masafa marefu, ambayo yamekuwa yakitishia usalama wa Marekani na washirika wake.
Mwezi Novemba, jaribio lingine kama hili lilifanyilka na ikaonekana ni ishara ya kuishinikiza Marekani.
Hakuna juhudi zozote zilizopigwa kati ya Korea Kaskazini na Marekani, baada ya Kim Jong Un kukutana na rais Donald Trump mwezi Februari nchini Vietnam na mazungumzo hayo kumalizika bila ya makubaliano yoyote.
Wiki iliyopota, Kim alisema Trump anahitaji fikra sahihi ili kuwezesha mazungumzo hayo kuedelea.
Marekani inataka korea Kaskazini kuharibu mitambo yake yote ya nyukulia, huku Korea Kaskazini ikitaka Marekani kuiondolea vikwazo.