- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KITUO CHA KUPOZEA UMEME CHATEKETEA KWA MOTO
KITUO cha kuzalisha na kusambaza umeme cha Mlandizi mkoani Pwani, kimteketea kwa moto asubuhi ya leo tarehe 30 Machi 2019.
Akizungumza na Waandishi muda mchache baada ya tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Wankyo Nyigesa, amesema, moto huo ulizuka majira ya saa 2.15 asubuhi na bado chanzo cha moto huo hakijajulikana
Amesema moto huo umeteketeza transform moja yenye megawati 24 ambayo ilikuwa ikizalisha na kusambaza umeme katika maeneo ya Bagamoyo, Kibaha na Mloganzila.
“Nikikuwepo eneo la tukio, hakuna madhara yoyote kwa binadamu isipokuwa jenereta limeteketea. Hadi sasa chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana, tunasubiri matokeo ya uchunguzi wa watalaamu,” amesema Kamanda Wankyo