Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 10:44 am

NEWS: KITUO CHA HAKI ZA BINAADAMU CHATAKA KUFUTWA ADHABU YA KIFO

Dar es salaam: Kituo cha sheria na haki za binaadamu (LHRC) kimeitaka serekali kufuta Adhabu ya kifo na badala yake kiunde sheria mbadala na kifo kama Kifungu cha maisha au adhabu nyingine yoyote. Kauli hiyo imezungumzwa na Kaimu mkurugezi Mtendaji wa kituo hicho Bi. Anna Henga katika kuadhimisha siku ya kupinga adhabu ya kifo duniani


Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne, Henga amesema "adhabu ya kifo inaondoa uwezekano wa mkosaji kujirekebisha na badala yake ni kuendeleza ukatili na kuondoa ubinadamu."

Henga amesema adhabu ya kifo inavunja misingi ya tamko la kimataifa la haki za binadamu la mwaka 1948 ambalo linasema kila mtu ana haki ya kuishi.

Amesema Tanzania inapaswa kujifunza kutoka kwa mataifa mengine duniani ambayo hayatekelezi adhabu ya kifo na badala yake kutoa adhabu mbadala kama vile kifungo cha maisha na kazi ngumu kwa watuhumiwa wa mauaji ili kulinda haki ya msingi ya kuishi.


Tanzania ni miongoni mwa nchi chache duniani kama vile China, Korea Kaskazini na Marekani ambazo zinaruhusu na kutekeleza adhabu ya kifo katika sheria zake.