Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 3:42 pm

NEWS: KISWAHILI CHAWEKWA KWENYE ORODHA YA LUGHA ZA MSHIKAMANO

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO ) limeitambua Lugha ya Kiswahili kama lugha itakayosaidia kukuza utangamano Barani Afrika wakati wa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Lugha Mama yenye kaulimbiu “Lugha Bila Mipaka” iliyofanyika jijini Paris.

Mjadala huo uliandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa kwa kushirikiana na Shirika la UNESCO wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Lugha Mama yaliyofanyika jijini Paris, Ufaransa.

Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa na Mwakilishi wa Kudumu katika UNESCO , Samwel Shelukindo akizungumza kwenye Mjadala kuhusu "Fursa na Changamoto za Kukitambua Kiswahili kama Lugha rasmi ya Bara la Afrika kwa ajili ya kukuza Utangamano.