- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KIONGOZI WA UPINZANI VENEZUELA AWATAKA WANAJESHI KUMUONDOA MADURO
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Venezuela Juan Guaido ametoa wito jana kwa jeshi la nchi hiyo kuasi na kumuondo rais Nicolas Maduro madarakani.
Kiongozi huyo aliongea katika ujumbe alioutoa kwa njia ya vidio akiwa pamoja na wanajeshi na mwanasiasa wa upinzani Leopoldo Lopez, ambaye alikuwa katika kizuwizi cha nyumbani kwamba mustakabali ni wa nchi hiyo, watu na majeshi ya ulinzi yako pamoja.
Baada ya vidio hiyo kutolewa nje ya kituo cha jeshi mjini Caracas, waungaji mkono wa Guaido walipambana na wanajeshi karibu na eneo hilo, na kusababisha watu 69 kujeruhiwa. Mamia kwa maelfu ya waungaji mkono Guaido pia walipambana na polisi katika barabara kuu ya Francisco Fajardo katika mji huo mkuu.
Baadhi ya waandamanaji walijeruhiwa baada ya gari ya jeshi la ulinzi kuwagonga.
Lakini alipoulizwa na shirika la habari la nchini Ujerumani la DW kwa simu jana, Guaido amesema majeshi ya ulinzi hayapo pamoja na Nicolas Maduro, yapo pamoja na mabadiliko na watu, pamoja na katiba.