- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KIONGOZI WA UPINZANI RWANDA AUWAWA KWA KUCHOMWA KISU
Kiongozi na Mwanasiasa maarufu wa upinzani nchini Rwanda Syridio Dusabumuremyi ameuwawa kwa kuchomwa kisu na watu wasiojulika , chama chake cha FDU-Inkingi kinasema.
Dusabumuremyi,ambaye ni mratibu wa chama hicho cha upinzani FDU-Inkingi, alikuwa kazini wakati aliposhambuliwa na wanaume wawili, kiongozi wa chama hicho Victoire Ingabire amesema
Kiongozi huyo alikuwa na duka la kuuza chakula katika kituo cha afya katika wilaya ya kati ya Muhanga.
Idara ya upelelezi nchini Rwanda imetuma ujumbe katika mtandao wa twitter kueleza kwamba imewakamata washukiwa wawili wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya Syridio Dusabumuremyi.
Katika ujumbe huo, idara hiyo imeeleza kwamba Dusabumuremyi Sylidio alichomwa kisu hadi kufa na watu wasiojulikana, aliuawa akiwa kazini katika kituo cha afya wilayani ya Muhanga.
Kwenye ujumbe uliofuata, idara hiyo ya upelelezi imeeleza kwamba katika uchunguzi wa awali, washukiwa wawili wamekamatwa kwa kuhusika na mauaji hayo.
Imeendelea kusema uchunguzi unaendelea kubaini dhamira ya mauaji hayo.
Bi Ingabire anasema mauaji ya Dusabumuremyi ni ya hivi karibuni kufuatia msururu wa mashambulio dhidi ya wafuasi wa chama chake kwa lengo la kuwatishia.
Miezi miwili iliyopita, Eugène Ndereyimana, mwakilishi wa chama cha FDU-Inkingi kutoka eneo la mashariki mwa Rwanda alitoweka. Mpaka sasa hajapatikana.
Mnamo Machi, Anselme Mutuyimana, msemaji wa chama hicho alitekwa na baadaye kukutikana amefariki msituni magharibi mwa nchi hiyo.
Mnamo 2016, mwanachama wa FDU-Inkingi Jean Damascène Habarugira aliuawa.
Bi Ingabire, ambaye ni mkosoaji mkubwa wa rais Paul Kagame, amesema chama chake kinalengwa kwasababu kinapania kutetea haki za raia wa Rwanda na uhuru wao.
"Lengo letu ni zuri na hatutaacha kulipigania hata wakafanya lolote," amesema.