- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KIONGOZI WA CHADEMA AFUNGULIWA KESI YA UHUJUMU UCHUMI
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA), Mkoa wa Songwe Bw. AYUBU Sikagonamo, amefutiwa kesi ya kukutwa na silaha, na kufunguliwa kesi nyingine ya uhujumu uchumi, kesi ambayo kwa mujibu wa sheria za Tanzania haina dhamana.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Baraza la vijana chadema BAVICHA kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, Sikagonamo amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Momba leo tarehe 18 Septemba 2019 na kubadilishiwa shitaka
Taarifa hiyo inaeleza kuwa, Sikagonamo alifikishwa mahakamani hapo na kufutiwa kesi ya awali ya kukutwa na silaha, kisha kukamatwa tena na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi Namba 10 ya mwaka 2019.
Taarifa hiyo ya BAVICHA inaeleza, kesi hiyo itaanza kusikilizwa tarehe 2 Oktoba 2019.
Sikagonamo alikamatwa na Jeshi la Polisi Julai mwaka huu, akituhumiwa kukutwa na silaha nyumbani kwake eneo la Mwaka katika Kata ya Chipaka, Tunduma mkoani Songwe.