- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KIONGOZI MKUU WA UPINZANI MWEUSI AJIUZULU SAUZI
Kiongozi mweusi wa chama kikuu cha upinzaji nchini Afrka Kusini Mmusi Maimane ametangaza kujiuzulu kwenye uongozi wa chama chake, cha Democratic Alliance.
Kujiuzulu kwake kunajiri siku tatu baada ya Herman Mashaba kujiuzulu kutoka chama hicho na pia kama meya wa mji wa Johannesburg.
Maimane ni mweusi wa kwanza kuongoza chama hicho, kwa muda mrefu kilichukuliwa kama chama cha Wazungu.
Chini ya uongozi wake, chama cha Democratic Alliance kilipata ushindi wa kihistoria katika uchaguzi serikali za mitaa miaka mitatu iliyopita.
Lakini chama hicho kinaendelea kugawanyika kati ya chama chenye itikadi ya mageuzi na chama kihafidhina.
Wengi hawakushangazwa na hatua hii ya kujiuzulu kwa Mmusi Maimane. Alikuwa ameweka usawa wa kikabila kwenye sera yake na alifanya kazi kwa kwa kuwashawishi watu weusi walio wengi nchini Afrika Kusini kujiunga na chama chake.
Mmusi Maimane amejiuzulu kufuatia mzozo unaotokana na ubaguzi wa rangi ndani ya chama chake Democratic Alliance.
Mmusi Maimane amesema chama hicho hakiweza tena kuwa chombo stahiki kwa malengo yake ya kuwepo taifa lenye umoja.
Maimane ameeleza kwamba alipata tabu katika kukifanya chama hicho ambacho kwa muda mrefu kimekuwa na wafuasi weupe wa kiberali - kuwavutia wapiga kura weusi.