- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KINANA NA MAKAMBA WAJISALIMISHA KUHOJIWA KAMATI YA MAADILI
Makatibu Wakuu Wastaafu Yusuf Makamba na Abdulrahman Kinana leo Februari 10, 2020 hatimaye wamefika kuhojiwa na Kamati ndogo ya Usalama na Maadili ya chama cha Mapinduzi CCM inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti Bara Philip Mangula.
Mahojiano hayo yamefanyika katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba Jijini Dar es salaam.
Kupitia Ukurasa Rasmi wa twitter wa Chama hicho umedhibitisha kuwa viongozi hao wawili wamefika leo asubuhi katika kamati hiyo licha ya kutokuwepo kwa maelezo ya Ziada yanayowahusu viongozi hao.
Hapo awali kulikuwepo na Taarifa kuwa viongozi hao wawili wa chama hicho waligoma kwenda kuhojiwa na kamati hiyo na taarifa za jana na leo asubuhi zilizoenea kupitia mitandao ya kijamii kuwa viongozi hao wameomba kuachana na Chama hicho.
Hofu bado ni kubwa juu ya Mustakabali wa chama hicho Juu ya hatima ya Viongozi wakongwe hao wa chama kikongwe Barani Afrika.
Picha Mbili zilizotolewa leo zilizoambatana na Taarifa ya Chama hicho moja inaonesha Katibu mkuu mstaafu Abdulrahman Kinana akiwa mbele ya kamti hiyo bila Katibu kuu mwenzake mstaafu Yusuph Makamba kuwepo katika kamati hiyo, huku picha ya pili ikimuonesha katibu mkuu wa sasa wa chama hicho akiongea kitu na Bw. Yusuph Makamba wakati makamba akiwa ndani ya Gari.
Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Bernard Membe Februari 6, 2020 alikuwa katika ofisi za makao makuu ya CCM mjini Dodoma asubuhi alihojiwa kwa saa 5 kuhusu tuhuma za kimaadili zinazomkabili.
Membe aliwasili katika ofisi hizo maarufu ‘white house’ akiwa katika gari aina ya Range Rover jeusi leo asubuhi, aliingia ndani ya jengo hilo saa 3:20 asubuhi.
Baada ya kuwasili, waziri huyo wa zamani wa Mambo ya Nje aliyevaa suruali nyeusi na shati lenye michirizi mieusi na kijani, alisalimiana na watu mbalimbali aliowakuta nje. Waandishi wa habari walifika mapema katika jengo hilo lakini hawakuruhusiwa kuingia ndani, kufuatilia kinachoendelea katika eneo walilopiga kambi lililopo nje ya uzio
Kunapokuwa na vikao katika jengo hilo, waandishi wa habari hutengewa eneo la kusubiri lakini leo hali ni tofauti. siku moja kabla ya kuhojiwa Membe alieleza kuwa kikao hicho kitakuwa muhimu kwake akitumia neno, “nilikuwa nakisubiri sana.”