Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 12:33 am

NEWS: KINACHOENDELA KWA SASA KENYA BAADA YA UCHAGUZI

Nairobi: Hali ya wasi wasi na ghasia zimeendelea kuwepo nchini Kenya leo Jumapili(13.08.2017) baada ya zaidi ya watu 11 kuuwawa katika maandamano ya ghasia, huku upande wa upinzani ukiendelea kudai kwamba kuchaguliwa tena kwa rais Uhuru Kenyatta kubatilishwe.

waungaji mkono wa mgombea wa upinzani aliyeshindwa Raila Odinga waliokuwa wakirusha mawe huku wakipambana na majeshi ya usalama siku ya Jumamosi katika maeneo ya ngome ya wapinzani upande wa magharibi wa nchi hiyo na maeneo ya mabanda katika mji mkuu Nairobi.


Jana Upande wa magharibi mwa Kenya , afisa wa polisi alisema mtu mmoja mwanamume alipigwa risasi na kufariki katika maandamano mjini Kisumu.

Bado haijawekwa wazi muungano wa vyama vya upinzani wa National Super Alliance NASA wa Raila Odinga utachukua hatua gani, lakini viongozi wa chama wamesema hawatarudi nyuma ama kupelela malalamiko yao mahakamani.

"Hatuta ogopa, hatuta kubali kupiga magoti," afisa wa NASA Johnson Muthama aliwaambia waandishi habari jana Jumamosi.

Akihutubia vyombo vya habari jana Jumamosi(12.08.2017), Muthama alionesha mfuko uliokuwa umejaa maganda ya risasi ambayo anadai yalitumiwa na majeshi ya usalama kuwauwa "Wakenya ambao hawana hatia" waliokuwa wakishiriki katika maandamano mitaani baada ya tangazo la ushindi wa Kenyatta siku ya Ijumaa usiku.

"Tunataka kuwahakikishia wananchi kwamba tuna nia, na dhamira, na uwezo wa kuhakikisha kwamba kura yako ni muhimu mwishoni mwa siku," amesema.