- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KIMBUNGA KENNETH KUENDA KIKAVURUGA ZAIDI MAKAZI YA WATU
Kimbunga Kenneth kimepiga pwani ya kaskazini ya Msumbiji usiku wa Alhamis ya jana huku mvua kubwa zikitarajiwa mara mbili zaidi ya dhoruba iliyoupiga mji wa Beira mwezi uliopita. Mtu mmoja amefariki huku makazi yakiharibiwa.
Kimbunga Kenneth kimelipiga jimbo la Cabo Delgado, kisha baadae kikaelekea jimbo la Sofala kaskazini mwa Msumbiji ambako ndiko uliko mji wa Beira ulioathiriwa zaidi na kimbunga Idai mwezi uliopita. Kimbunga Idai kiliwaua mamia ya watu na kusababisha maelfu kukosa makazi nchini Msumbiji, Malawi na Zimbabwe.
Kwa mujibu wa shirika la Mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP, kimbunga Kenneth kinatarajiwa kusababisha mvua kubwa katika kipindi cha siku 10 zijazo ikiwa ni mara mbili zaidi ya zile zilizonyesha wakati wa kimbunga Idai.
Katika taarifa yake WFP imesema wilaya nne za Cabo Delgado za Macomia, Mocimboa da Praia, Muidumbe na Palma, zinatazamiwa kuathirika zaidi kutokana na upepo unaotarajiwa kupiga kwa zaidi ya kilometa 120 kwa saa. Kwa mujibu wa WFP, kiasi ya watu 112,000 wako hatarini na kwamba shirika hilo lina zaidi ya tani 1,000 za msaada wa chakula tayari kuwasaidia watakoathirika.
Serikali ya Msumbiji imeanza kuwalazimisha watu kuondoka katika maeneo yaliyoko hatarini siku mbili kabla ya kimbunga kupiga. Jumla ya watu 30,000 wamehamishiwa katika maeneo salama, huku shule zikitumika kuwahifadhi watu hao. Rais Filepe Nyusi amewahutubia wananchi kupitia televisheni akiwataka kuwa watulivu. Kimbunga hicho pia kilisababisha maafa katika visiwa vya Comoro. Mkurugenzi mkuu wa ulinzi wa kiraia visiwani humo Ismael Mogne Daho, amethibitisha vifo vya watu watatu. Mmoja wa wakazi wa visiwani humo aliyeathirika anasema.
''Usiku ulikuwa wa hofu sana matumboni mwetu. Kuanzia saa nne usiku na kuendelea, hatukulala. Hali ya hewa ilikuwa mbaya sana na hatukujua wapi pa kwenda katika kiza cha namna ile na watoto. Mvua kubwa ilinyesha na upepo mkali. Miti ilianguka, hapo palikuwa na muembe, tulikuwa tukikaa chini yake lakini uliangushwa''.