Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 2:24 pm

NEWS: KIMBUNGA CHA IRMA CHAWA TISHIO KUBWA MAREKANI

Florida: Marekani yaendelea kukubwa na majanga makubwa ya asili baada ya kimbunga cha hurricane kuikumba Houston, Kimbunga Irma kimepiga aridhi ya Florida katika eneo la Marco Island magharibimwa jimbo hilo. Baada ya kuwekwa katika kundi la 3, kwa kiwango cha 5 cha janga la hatari, baadaye kimbunga Irma kilipunguzwa na kuwekwa katika kundi la 2.

Wakati ambapo utulivu ukirejea hatua kwa hatua katika mji wa Miami, bahari ya Tampa, mji wa pwani ya magharibi ya jimbo la Florida, inachukuliwa kuwa eneo lilio katika mazingira magumu zaidi nchini Marekani. Donald Trump ametangaza kwamba Florida iko katika hali ya janga la asili.

Kimbunga Irma kimepiga visiwa vilivyo kusini mwa jimbo la Florida nchini Marekani kikiwa katika kiwango cha nne, kwa mujibu wa watabiri wa hali ya hewa.

Viwango vya maji tayari vimeanza kuogezeka katika maeneo ya pwani ya Florida, eneo ambalo linatarajia kimbunga kikubwa kuwasili.


Taharuki na hatma ya baadaye ya mji wa Tampa, ambao unakabiliana ana kwa ana na njia inakopitia kimbunga hicho, haijulikani.

Kimbuga hicho kimepiga visiwa vilivyo nyanda za chini na upepo wa kasi ya hadi kilomita 209 kwa saa kabla ya kuelekea kaskazini magharibi kwa ghuba ya Florida.


Watu zaidi ya Milioni sita wameshauriwa kuhama Florida, wakati huu mji wa Miami ukifurika maji.

Kimbuga hiki kilianzia katika visiwa vya Carribean mwishoni mwa wiki iliyopita.

Maelfu ya watu wamepoteza mali zao kutokana na janga hili.