Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 3:48 pm

NEWS: KIM AYATAKA MAJESHI YAKE KUJIWEKA TAYARI KWA MABAMBANO NA MAREKANI

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ameliamrisha jeshi lake kuimarisha nguvu ya mashambulizi mara moja tayari kwa mapambano dhidi ya Marekani, huku akiagiza kurushwa kwa kombora jingine.

Image result for Kim jong un reaction to ship seized

Kim ametoa amri hiyo baada ya kupata habari kwamba Marekani imeikamata meli yake kubwa ya mizigo ya nchi hiyo juzi Alhamisi kwa madai kuwa ilikuwa inasafirisha shehena ya makaa ya mawe kinyume cha sheria za kimataifa.

Kim ameyataka majeshi yake yajiweke tayari kwa mapambano ya hivi karibuni, ambapo haijafahamika kwamba Korea inataka kufanya mashambulizi dhidi ya marekani moja kwa moja au kwa washirika wake.

Image result for Kim jong un reaction to ship seized

Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa hatua ya marekani kuikamata meli ya Korea Kaskazini kuenda ikazua uhasama mkubwa kuwahi kushuhudiwa, kiasi ambacho huenda kikaighadhibisha nchi hiyo na kuamua kufanya maamuzi magumu dhidi ya Marekani na Washirika wake.

Wizara ya sheria ya Marekani imesema meli hiyo ya tani,17,061 inayoitwa Wise Honest ndiyo kubwa kabisa ya Korea Kaskazini ambayo kwanza ilizuiwa na Indonesia mwaka uliopita na sasa imekamatwa na Marekani.

Mivutano imejitokeza katika muktadha wa mkwamo wa mazungumzo baina ya kiongozi huyo wa Korea Kaskazini na Rais wa Marekani Donald Trump. Mazungumzo baina ya viongozi hao wawili yalimalizika bila ya kufikiwa mapatano walipokutana kwa mara ya pili nchini Vietnam.