Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 2:43 pm

NEWS: KIM APANDA MLIMA MTAKATIFU KWA KUTUMIA FARASI YAKE

Raisi wa Korea kaskazini Kim Jong-un amepanda mlima mrefu kuliko yote nchini humo kwa kutumia farasi.

Hii si mara ya kwanza kwa kiongozi huyo kufanya hivyo kwani alishawahi kupanda kilele urefu wa 2,750m huku dhumuni likiwa ni kufanya matangazo muhimu.

Mlima huo ni mahali ambapo baba wa kiongozi huyo wa Korea kaskazini alizaliwa huku pia ni kati ya vivutio vya nchi hiyo.

Kitendo cha kiongozi huyo kupanda mlima wa Paektu ni kitendo kikubwa cha kihistoria.

Kiongozi huyo ametafakari hatua iyo ya kupanda mlima Paektu kama kuongoza nchi hiyo huku akisema inahitaji kuwa imara kama mlima huo.

Mara ya mwisho Kim Jong-un kupanda mlima Paektu kumeleta matokeo makubwa na mipango mikubwa iliyofanywa na kiongozi huyo juu ya nchi hiyo.