Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 8:43 pm

NEWS: KILICHOJIRI KESI YA ALIYEMUUA MKEWE KWA KUMCHOMA NA MOTO

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, leo Jumanne Septemba 10 imeendelea kusikiliza kesi ya mauaji inayomkabili mfanyabiashara Khamis Saidy, anayekabiliwa na mashtaka ya kumuua na kisha kumchoma moto Mke wake Naomi Marijani.

Akizungumza katika Mahakamani hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Salum Ally, Wakili wa Serikali Wankyo Simon amesema kuwa, upelelezi wa kesi hiyo upo katika hatua za mwisho ili kuipatia mahakama hiyo nyaraka na hatimae kesi hiyo kupelekwa Mahakama Kuu.

Baada ya maelezo hayo, mshtakiwa aliiomba mahakama kupatiwa hati ya mashtaka yanayomkabili ambapo wakili Wankyo, aliahidi kumpatia na kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 24, itakapofikishwa mahakamani hapo tena kwa ajili ya kutajwa.

Mfanyabiashara huyo anakabiliwa na mashtaka ya kuua kwa kukusudia, ambapo inaelezwa alitekeleza kosa hilo Mei 15, 2019, mara baada ya kumuua kisha kumchoma na moto wa magunia mawili ya mkaa mke wake Naomi Marijani, kisha kuyachukua mabaki ya mwili huo na kwenda kuyafukia shambani kwake Mkuranga.

mara baada ya mauaji hayo, Khamis Said Luongo, aliuchukua mwili wa Naomi na kuuweka kwenye shimo alilochimba kwenye banda la kufugia kuku. Baadaye aliweka mkaa gunia mbili na mafuta ya taa na kisha kuwasha moto uliowaka muda mrefu sana na mwili wote kuteketea kuwa majivu.” Anaongeza,


kutokana hapo, Meshack aliupakia mwili wa marehemu Naomi kwenye gari lake na kuufikisha kwenye shamba analolimili, lililopo eneo la Vikindu, wilayani Mkuranga, mkoani Pwani. Akachimba shimo na kisha kuufikia. Juu ya eneo hilo, akapanda mgomba.” Naomi Marijani (Sadra), mfanyabiashara na mwenyeji wa mkoa wa Kilimanjaro, ameacha mtoto mmoja, aitwaye Grecious mwenye umri wa miaka saba.