- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KIKWETE ATAKA KUPUUZWA WANAOZUSHA UWONGO KIFO CHA MENGI
Rais Mstaafu wa awamu ya nne, nchini Tanzania Jakaya Mrisho kikwete amewataka watanzania wote kutosikiliza na kupuuzilia mbali wanaozusha "maneno ya uongo" kuhusu kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa IPP Media, Reginald Mengi huku akisema kuwa kufanya hivyo ni kuichanganya Jamii
Kikweti ametoa kauli hiyo leo May 4, 2019 mara baada ya kujumuika na watanzania wengine kuwapa pole Wafiwa.
"Sisi wengine tuendelee kuwa watulivu, tuache uwongo, tuache kusikiliza yasiyo kuwepo, kuichanganya jamii. "Kama kweli tunampenda Mengi haya mengine ya kutunga tunga tuachane nayo" amesema Rais Kikwete
Pia kikwete amewataka wananchi kusubiri ukweli kutoka kwa ndugu waliopo Dubai ambao walikuwepo wakati marehemu anaaga Dunia.
Marehemu Reginald Mengi alifariki May 2, 2019 nchini Dubai ambapo alikuwepo kwa mapumziko na baadae kufariki mara baada ya kuumwa ghafla.
Kupitia ukurasa wake wa twitter kikwete mara baada ya kupata taarifa ya kifo cha mzee mengi aliandika ujumbe wa masikitiko juu ya kifo hicho
" Nimepokea kwa huzuni kubwa taarifa ya kifo cha ndugu yetu Dkt. Mengi.Taifa limepoteza mzalendo wa kweli na mfanyabiashara mahiri. Tutamkumbuka kwa mchango wake mkubwa aliyoutoa kwa maendeleo ya taifa letu na moyo wake wa upendo na huruma kusaidia jamii na hasa watu wasiojiweza." aliandika kikwete