- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KIJANA AFUNGWA 30 JELA KWA KUMBAKA NA KUMTIA MIMBA MWANAFUNZI
Mahakama ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu imemuhukumu Sunzu Mpangala mwenye umri wa miaka 27 kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kumbaka na kumsababishia ujauzito mwanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Maswa.
Mbele ya Hakimu mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Maswa, Tumain Marwa, Mwendesha mashtaka Inspecta, Nassib Swedi aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo tarehe 12.6.2018 majira ya saa 11 jioni huko katika Kijiji cha Igunya, Kata ya Shishiyu.
Mwendesha mashtaka huyo aliendelea kuiambia mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa Sunzu Mpagala anatuhumiwa kwa kosa hilo mwanafunzi huyo wa kidato cha sita wa Shule ya Wasichana Maswa.
Awali inadaiwa kuwa mtuhumiwa Mpangala alikuwa akimfundisha masomo ya ziada mwanafunzi huyo wakati wa likizo akiwa anasubiria ajira kutoka Serikalini kwani yeye ni mhitimu wa Shahada ya Elimu katika Chuo Kikuu UDOM.
Mwendesha mashtaka Swedi aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo kinyume na Kifungu Namba 60A (3) cha Sheria ya Elimu Sura ya 353 kama ilivyofanyiwa Marekebisho ya Sheria ndongo Namba 2 ya mwaka 2016.
Mtuhumiwa alipopewa nafasi ya kujitetea mahakamani hapo alikiri kutenda kosa hilo na kuiomba mahakama ijaribu kumpunguzia adhabu kwa kuwa yeye hana wazazi na anategemewa na familia, hoja ambayo haikumsaidia na hivyo kumlazimu mwendesha mashtaka kuiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mtuhumiwa huyo ili iwe fundisho kwake na wengine wenye tabia kama hizo kwani wamekuwa wakikatisha ndoto za wanafunzi.