Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 2:22 pm

NEWS: KIJANA ADAIWA KUFARIKI DUNIA AKIWA MORO APATIKANA AKIWA HAI DAR

DODOMA: Wananchi pamoja na viongozi wa kata ya kizota manispaa ya Dodoma wamejikuta wakigubikwa na hali ya sintofahamu mara baada ya kukumbwa na tukio waliloliita kuwa ni la ajabu baada ya kijana wa familia moja kufariki dunia mkoani Morogoro na mwili wake kuzikwa mkoani hapa na kisha kupatikana akiwa hai mkoani Dar es salaam.

Akisimulia tukio hilo Mama wa familia hiyo Bi. Sarah Michael amesema walipokea taarifa za kifo cha kijana wake Seif Ramadhan kutokea mjini Morogoro siku ya jumanne ya wiki iliyopita ndipo waliposafirisha kwa ajili ya mazishi lakini mara baada ya maziko akashangazaa kupokea taarifa za kijana wake akiwa hai

Kwa upande wake mjomba wa kijana huyo Idd Salum ambaye alihusika kwenda kuhakiki mwili mjini morogoro pamoja na bi.maria daniel ambaye ni mama mdogo,wao pia wamebaki katika hali ya sintofahamu kwani hadi sasa hawaamini kilichotokea

Hata hivyo MUAKILISHI imepata nafasi ya kuzungumza na kijana Seif Ramadhan aliyesemekana kufariki na kisha kuonekana tena yeye amewaomba wananchi waamini kuwa yeye ni mzima na wala hajawahi kufariki

Pamoja na kushangazwa na tukio hilo viongozi wa kata hiyo akiwepo diwani wa kata hiyo Mh.Yered Jamal na Mwenyekiti wa mtaa wa relini Omary Hamis wamewashauri wananchi nchini kote kuwa makini katika utambuzi wa miili ya ndugu zao pindi wanapopata matatizo