Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 3:51 am

NEWS: KIGOMA YAINGIA KWENYE HISTORIA YA KUZALISHA UMEME MWINGI E.A.C

Kigoma: Mbunge wa Kigoma Ujiji Zitto Zuberi kabwe Jana alitembelea kwenye eneo la ufungwaji wa sola zenye uwezo wa kuzalisha umeme wa 5M/W ambao utaingia kwenye Gridi ya kigoma, kupitia ukurasa wake wa Facebook Zitto aliandika kuwa baada ya ukamilikaji wa mradi huo kigoma utakuwa mji wa Pili Afrika mashariki kwa kuwa na umeme mwingi wa Jua baada ya Rwanda.


"Kigoma kuzalisha Umeme wa Jua mwingi kuliko Mji wowote Afrika Mashariki ( isipokuwa Rwanda). Ambapo Umeme 5MW utazalishwa na kuingizwa kwenye gridi ya Kigoma." alisema Zitto


Zitto alisema kuwa wanakusudiwa baadae kuzalisha umeme wa 13M/W " Tunaweka zingine 13MW ambapo 3MW zitakuwa Kwa ajili ya kuendesha mradi wa Maji na hivyo kuepusha kupandisha bei za Maji Kwa wananchi wetu na 10MW kuingia gridi ya Kigoma na hivyo kuwa 100% mji unaoendeshwa Kwa nishati jadidifu, The Greenest City in Africa."