Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 11:07 pm

NEWS: KIFO CHA NDESAMBURO PIGO KWA CHADEMA

DODOMA: CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupokea kwa mshutuko mkubwa wa kifo cha Mwasisi wa chama hicho na mbunge wa mstaafu wa jimbo la Moshi Philimoni Ndesamburo(84).

Ndesamburo alikuwa mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini kwa mfululizo wa miaka 15 na aliamua kustaafu kwa heshima huku akiendelea kuimalisha chama pamoja akiwa na nafasi ya kuwa mwenyekiti wa kanda katika mkoa wa Kilimanjaro.

Mauti yamemkuta mwasisi wa chama hicho akiwa katika maadalizi ya kuandika cheki ya kiasi cha sh. Milioni 3.5 kama sehemu ya rambirambi kwa ajili ya wanafunzi 35 waliopata ajari na kupoteza maisha katika shule ya msingi ya Lucky Vicent.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Bunge, Mwenyekiti wa Chadema Taifa,Freeman Mbowe,amesema kifo cha Mwasisi huyo ni msiba mkubwa kwa wanachadema na wakazi wa Mji wa Moshi kwa ujumla kutokana na jinsi alivyoweza kujenga ushirikino na umoja wakati wa utawala uongozi wake.

Akielezea juu ya kicho chake Mbowe alisema mwasisi huyo alikuwa katika vikao wa baraza kuu la Chadema vilivyofanyikia mjini Dodoma aliweza kurejea moshi akiwa na nguvu zake bila kuwa na viashiria vyovyote vya ugonjwa.

Mbowe amesema mwasisi huyo baada ya kumaliza vikao vya baraza kuu la Chadema, alirudi moshi na jana (Juzi) alimpigia simu meya wa Jiji la Arusha Kalist Lazaro ili afike nyumbani kwake moshi kwa ajili ya kumpatia rambirambi kwa ajili ya watoto waopata ajari na kupoteza maisha katika shule ya msingi Lucky Vicent.

Amesema Ndesamburo alimpigia meya huyo akitaka wakutane saa asubuhi jana leo(jana) na Meya alifika nyumbani kwa Ndesamburo saa nne kamili ambapo walianza kufanya mazungumzo ya kawaida pamoja na mazungumzo kwa ajili ya chama.

Aidha Mbowe amesema wakati wa maongezi hayo alitaka kujua waathirika wa ajari hiyo walikuwa wangapi na ndipo Meya alipomweleza kuwa walikuwa 35 ambapo alikuwa amekubali kutoa kiasi cha sh.laki moja kwa kila mwathirika kiasi cha jumla y ash. Milioni 3.5.

“Wakati Ndesamburo akianza kuandika kitabu cha cheki kwa lengo la kumkabidhi Meya kama mchango wa rambirambi kalamu ilimdondoka na kumfanya meya kumsaidia kwa lengo la kumuokotea kalamu hiyo lakini bado nguvu ziliendelea kumwishia jambo ambalo lilipelekea Meya pamoja na familia kuanza kumsaidia na kumkimbiza katika hospitali ya KCMC.

“Hata hivyo madaktari walimpokea na kuanza kumpatia msaada wa kumpatia huduma ya kumsaidia kupumua kwa mashine na majira ya saa tano kasorobo Ndesamburo alikata roho na kupoteza maisha,hivyo taarifa za msiba tumezipokea kwa masikitiko makubwa, na ifahamike kuwa Lucy Owenya ambaye ni mbunge wa Viti Maalum na ni mtoto wake alikuwa bungeni akichangia.

“Baada ya kupokea taarifa hizo tumefanya kazi ya kumtoa bungeni kwanza na kumpeleka nyumbani kwake area ‘D’ kwa ajili ya kushughulika na taratibu nyingine kwa kuzingatia kuwa mwasisi huyo pamoja na umuhimu ndani ya chama taratibu za kumsindikiza mzee wetu tunazifanya na taratibu zote zinafanyika” alieleza Mbowe.

Kabla taarifa ya msiba Lucy Owenya (Chadema) akichangia aliitaka serikali ieleze ni wapi zilipo fedha ambazo serikali ilizizuia kwa maana ya DESI.

Owenya amesema serikali imeshindwa kutoa majibu ambayo yanaonesha ni wapi fedha za DESI zimepelekwa na kuhoji kuwa au pesa hizo zimeenda kufanya shughuli za serikali kama ilivyo kwa fedha za rambirambi za Arusha.