- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KESI YA WAMBURA BADO HAKIJAELEWEKA, ARUDISHWA RUMANDE
Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa makamu wa rais wa TFF, Michael Wambura imepigwa tena kalenda kutokana na Wakili wa Serekali kudai kuwa upelelezi haujakamilika.
Kwa mujib wa Wakili wa serikali Wakili Fatma Waziri amedai kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi haujiamilika wakaomba tarehe nyingine ya kutajwa na kwamba upelelezi ukikamilika wataeleza.
Ufafanuzi huo wa Wakili Fatma ameueleza leo Alhamisi Mei 23 katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu mbele ya hakimu mkazi mfawidhi, Kelvin Mhina wakati kesi hiyo ilipokuwa ikitajwa.
Mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Juni 4 kwa kutajwa na mshtakiwa anaendelea kusota gerezani kwasababu mashtaka yake hayana dhamana.
Wambura anakabiliwa na mashtaka 17, yakiwemo mawili ya kutakatisha jumla ya Sh. milioni 100.9.
Awali ilidaiwa mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka 17, yakiwemo 13 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, mawili ya kutakatisha fedha, moja la kughushi na moja la kuwasilisha nyaraka ya kughushi TFF.