- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KESI YA VIGOGO 5 WA SEREKALI AKIWEMO HAKIMU YAGONGA MWAMBA
Washtakiwa watano wanaokabiliwa na KESI ya utakasaji fedha na uhujumu uchumi, akiwemo Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha Bernad Nganga ,Mwanasheria wa hifadhi za Taifa (TANAPA)Maneno Mbunda na mwanasheria wa serikali Fortunatus Mhalila imezidi kupigwa kalenda kwa sababu ya kusubiri jalada kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP).
Akiomba kuahirishwa kesi hiyo jana septemba 17 mbele ya Hakimu Rose Ngoka wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha,Wakili wa Serikali Eliainenyi Njiro amesema kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa japo upelelezi umekamilika.
"Mheshimiwa kesi hizi tunaomba tarehe nyingine sababu jalada bado lipo kwa DPP na upelelezi umekamilika,"alisema.Hakimu Ngoka amesema kesi hiyo anaiahirisha hadi Oktoba Mosi mwaka huu itakapotajwa tena.
Washitakiwa hao na wenzao Nelson Kangero na Tumaini Mdee mbali na mashitaka hayo pia wanakabiliwa na mashtaka mengine tisa.
Awali washitakiwa hao walifikishwa Mahakamani hapo Mei sita mwaka huu na kusomewa mashitaka 11 na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Javelin Rugahuruza, yakiwemo ya kujihusisha na rushwa,kughushi na kujipatia mali kwa njia ya rushwa kati ya Juni Mosi mwaka 2018 na Aprili 15 mwaka huu katika maeneo mbalimbali.
Aidha mashitaka mengine waliosomewa waliyotenda katika kipindi hicho ni kuchukua rushwa ya Sh.milioni 31.5 toka kwa Kangero,utakasaji fedha ya Sh.milioni 31.5 kughushi nyaraka za uongo za nyara ya Serikali za kilo 15 za meno ya Tembo ya Sh.milioni 9.8
Nae mshitakiwa Kangero anakabiliwa na Shitaka la uhujumu uchumi kwa kukutwa na meno ya Tembo vipande 15 vya thamani ya dola za Kimarekani milioni 15,000 sawa na fedha za kitanzania zaidi ya Sh.milioni 108 bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori