- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KESI YA UCHOCHEZI YA ZITTO KABWE YASHINDWA KUENDELEA TENA
Dar Es Salaam. Kesi ya "uchochezi" ya Jinai Na. 327 ya Mwaka 2018 inayomkabili Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini Ndg. zitto kabwe katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imekwama kuendelea kusikilizwa baada ya hakima wa serekali kudai shahidi aliyepaswa kutoa ushahidi yupo kwenye oparesheni maalumu ya Jeshi la Polisi.
Baada ya mahakama kuelezwa hivyo hakimu katika kesi hiyo amepanga siku mbili mfululizo, kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka katika kesi ya uchochezi inayomkabili, Mbunge huyo. Kesi hiyo itaanza kusikilizwa kuanzia April 24 hadi 25, mwaka huu ambako Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi, katika mahakama hiyo.
Uamuzi huo umetolewa leo, April 9, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shaidi, baada ya upande wa mashtaka kuieleza mahakama kuwa shahidi aliyepaswa kutoa ushahidi yupo kwenye oparesheni maalumu ya Jeshi la Polisi. "Kesi hii nitaisikiliza kwa siku mbili mfululizo kuanzia April 24 hadi 25, hivyo upande wa mashtaka mjipange kuleta mashahidi wa kutosha ili kesi hii iweze kumalizika muda uliopangwa," alisema Hakimu Shaidi.
Awali, wakili wa Serikali Mkuu, Tumaini Kwema akisaidiana na Faraji Nchimbi alidai kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kuanza kusikiliza ushahidi, lakini shahidi aliyepaswa kutoa ushahidi yupo kwenye oparesheni maalumu ya Jeshi la Polisi. "Kwa bahati mbaya shahidi ambaye tulimtegemea kuja kutoa ushahidi yupo katika operesheni maalum ya Jeshi la Polisi" amedai Kweka.
"Kutokana na hali hiyo, tunaiomba mahakama itupe tarehe fupi ili tuweze kuendelea na usikilizwaji wa ushahidi," amedai Kweka.
Hakimu Shaidi baada ya kusikiliza hoja hizo, aliahirisha kesi hiyo hadi April 24 na 25, 2019 itakapoanza kusikilizwa na kuutaka upande wa mashtaka kuhakikisha kuwa wanaleta mashahidi wa kutosha.
Zitto alifikishwa Mahakama ya Kisutu kwa mara ya kwanza, Novemba 2, 2018 kujibu mashtaka matatu ya uchochezi katika kesi ya jinai namba 327/2018. Katika kesi ya msingi, Zito anadaiwa kutenda makosa hayo, Oktoba 28,2018 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya chama cha ACT Wazalendo.
Katika shtaka la kwanza, anadaiwa kuwa siku hiyo akiwa katika mkutano na waandishi wa habari kwa nia ya kuleta chuki miongoni mwa wananchi wa Tanzania dhidi ya Jeshi la polisi alitoa maneno ya uchochezi. Alitoa maneno ya uchochezi kuwa "watu ambao walikuwa ni majeruhi katika tukio la mapambano baina ya wananchi na polisi, wakiwa wamekwenda hospitali kupata matibabu katika kituo cha afya cha Nguruka, polisi wakapata taarifa kuwa kuna watu wanne wamekwenda hospitali kituo cha afya Nguruka kupata matibabu wakawafuata kule wakawaua."