Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 11:31 pm

NEWS: KESI YA UCHOCHEZI YA HALIMA MDEE YAGONGA MWAMBA TENA

Dar es Salaam: Kesi inayomkabili Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee ya kutoa lugha chafu dhidi ya Rais John pombe Magufuli imeshindwa kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na wakili wa Serikali anayeshunghulikia kesi hiyo kutokuwapo mahakamani hapo.

lakini Wakili wa Serikali, Daisy Makakala ameiambia mahakama mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ameeleza kesi hiyo ilipelekwa mahakamani hapo leo kuomba kuahirishwa kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake. “Tunaye shahidi ndugu, Abdi Chembeya lakini kwa leo hatutaweza kuendelea na kesi hii kutokana na sababu zilizopo nje ya uwezo wetu, tunaomba tarehe nyingine," ameomba Makakala.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Simba alitaka Mahakama ielezwe sababu za kesi hiyo kutoendelea wakati shahidi yupo.

Katika majibu yake, wakili Makakala ameeleza walikuwa waendelee lakini wakili aliyekuwa akisimamia kesi hiyo tangu mwanzo hayupo.

Kwa upande wake, wakili wa utetezi, Hekima Mwasipu amesema bado miezi minne tu kesi hiyo itimize miaka miwili tangu ianze kusikilizwa na kuiomba Mahakama kuahirisha kesi hiyo kwa mara ya mwisho.

Hakimu Simba amesema sababu zilizotolewa ni za msingi na kuahirisha kesi hiyo na kupanga itaendelea tena Aprili 16 na 24. Hadi sasa mashahidi watatu wa upande wa mashtaka wameshatoa ushahidi.

Julai 3, 2017 katika ofisi za makao makuu ya Chadema zilizopo mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni, Mdee alitamka maneno mabaya dhidi ya Rais John Magufuli akisema: “Anaongea hovyo, anatakiwa afungwe breki” kitendo kinachodaiwa kuwa ni kumdhalilisha Rais na kuhatarisha uvunjifu wa amani.