- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KESI YA UBADHIRIFU YA WAZIRI NETANYAU KUANZA MARCH 17
Kesi ya ubadhirifu inayomsubiri Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyau, itaanza kusikilizwa kortini tarehe 17 Machi, wiki mbili tu baada ya Israel kufanya uchaguzi wa tatu wa kitaifa katika muda usiotimia mwaka mmoja. Mbali na kesi mahakamani, Netanyahu
vile vile anapigana juu chini kuuokoa mustakabali wake kisiasa, wakati akikiongoza chama chake cha Likud katika uchaguzi wa Machi Mbili, kufuatia chaguzi nyingine wa Aprili na Septemba mwaka jana ambazo hazikudhihirisha mshindi wa wazi.
Wizara ya sheria imesema katika tangazo lake kuwa Netanyahu atalazimika kuhudhuria kikao cha mahakama cha Machi, kusikiliza mashtaka dhidi yake yatakayosomwa na jopo la majaji watatu.
Mashtaka hayo ni pamoja na kupokea rushwa, kughushi na kuvunja uaminifu. Netanyahu ambaye ni waziri mkuu wa kwanza wa Israel kushtakiwa akiwa madarakani, amezikanusha shutuma hizo akisema ni za uongo.