- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KESI YA TUNDU LISSU YASHINDWA KUENDELEA
Kesi inayomkabili aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, na Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu Lissu imeshindwa kuendelea tena baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuwasilisha jalada wakati kesi hiyo ilipoitishwa kwa ajili kusikilizwa.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana ilitarajia kusikiliza maombi yaliyowasilishwa na wadhamini wa mshtakiwa huyo wakiomba mahakama kutoa hati ya kumkamata kwa kuwa wao wameshindwa.
Wakili wa Serikali Ester Martin mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amedai kuwa mwendesha mashtaka anayesikiliza shauri hilo hayupo hivyo kuomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kusikilizwa.
Baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha hoja hiyo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Aprili, 23 mwaka huu, kwa madai kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuwasilisha jalada la kesi hiyo mahakamani hapo.
Katika kesi ya msingi Lissu anakabiliwa na kosa la kula njama na mhariri wa Gazeti la Mawio ili kutoa machapisho kwenye gazeti yenye maneno ya uchochezi.
Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji was Kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh.