- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KESI YA TALAKA YA DC WA CHEMBA YASHINDWA KUENDELEA
Dar es Salaam. Leo Agosti 18, 2019 Mahakama ya Mwanzo ya Ukonga, Jijini Dar es Salaam imeshindwa kuendelea kuisikiliza kesi ya madai ya talaka namba 181 ya mwaka 2019 iliyofunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga kwa kuwa mzee mmoja wa baraza la wazee wanaoshiriki kusikiliza kesi hiyo kufiwa.
Kufuatia hali hiyo, Hakimu anayeisikiliza kesi hiyo, Christina Luguru ameiahirisha mpaka Agosti 27, 2019 ambapo itaendelea kusikilizwa.
Katika kesi hiyo, Odunga alifungua dhidi ya ndoa yake ya Kikristu ambayo aliifunga na Medilina Mbuwuli ambayo ilifanikiwa kupata mtoto wa kike ambaye kwa sasa anasoma kidato cha sita.
Kwenye kesi hiyo, Medilina Mbuwuli ambaye ni mke wa ndoa ya Kanisani wa mkuu huyo wa wilaya Odunga anadai mumewe hajawahi kutoa matunzo ya mtoto wao wa kike mwenye umri wa miaka 18 tangu akiwa chekechea hadi sasa yupo kidato cha sita.
Hata hivyo, alieleza licha ya mumewe utotoa matunzo hayo, hayupo tayari kupewa talaka kwa sababu ndoa yao ni takatifu ya kanisani na kwamba bado anampenda mume wake na anajua hizo ni changamoto tu zimempitia.
Katika kesi hiyo, Mbuwuli alieleza yeye na mumewe tangu wafunge ndoa mwaka 1998 na kupata cheti cha ndoa A no 00140917 hawajawahi kuchuma mali yoyote na hana mgogoro na kwamba Odunga amechuma mali na kahaba wa nje ya ndoa.
Hata hivyo alidai katika ndoa yao Odunga amekuwa akikaa kwake akiwa hana pesa na akipata pesa anaishi kwa mwanamke huyo wa nje ya ndoa na kwamba ana mashahidi wa kutosha.
Aliongeza mumewe ana tabia ya kwenda kwake kila Julai muda ambao hata serikali haina pesa.
Kuhusu mtoto Mbuwuli aliomba mahakama iamuru Odunga amlipe gharama alizotumia kumtunza mtoto wao huyo wa kike mwenye umri wa miaka 18 tangu akiwa chekechea hadi alipo sasa kidato cha sita na kwamba risiti ambazo zinaonesha gharama za ada alizotumia anazo
Pia ameiomba mahakama iamuru Odunga amuhudumie yeye kama mke na mtoto wao.
Kwa upande wake, Odunga ambaye ni mdai katika kesi hiyo alidai kuwa Mbuwuli ni mke wake wa ndoa ya Kikristu na kwamba walitengana rasmi mwaka 2003.
Alidai wana mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 18 sasa ambaye anaishi na mama yake na hakuna mali yoyote waliyochuma.
#MCL DIGITAL