- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KESI YA MDEE YAKUTOA LUGHA CHAFU DHIDI YA RAIS MAGUFULI YAHAIRISHWA
Dar es Salaam. Kesi ya kutoa lugha chafu dhidi ya Rais John Magufuli inayomkabili Mbunge wa Kawe, Bi Halima Mdee imelazimika kuhairishwa hadi Aprili 28, 2020 baada ya mdhamini wa Mbunge huyo Bw Faris Lupomo kuielezea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa mshtakiwa huyo ameshindwa kufika mahakamani hapo kutokana na kuwa na maumivu makali katika mkono wake uliovunjika.
Mdee alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Julai 10, 2017.
Mdhamini huyo amesema hayo baada ya Wakili wa Serikali, Silyvia Mitanto kueleza mahakamani leo Jumatano Aprili Mosi, 2020 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutolea uamuzi lakini mshtakiwa hayupo mahakamani hapo.
Kutokana na maelezo hayo Lupomo aliieleza mahakama hiyo kuwa Mdee alikuwa anasafiri akitokea mkoani Dodoma kuja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudhuria kesi hiyo pamoja na kliniki kwa ajili ya mkono wake uliovunjika.
"Kwa bahati mbaya akiwa safarini akitokea Dodoma kuja Dar es Salaam mkono wake umeshtuka na anasikia maumivu makali sana hivyo ameshindwa kufika mahakamani,"alieleza Lupomo.
Baada ya maelezo hayo Hakimu Simba aliahirisha shauri hilo hadi Aprili 28, 2020 kwa ajili ya kutolewa uamuzi.
Katika kesi ya msingi inadaiwa kuwa Julai 3, 2017 katika ofisi za makao makuu ya Chadema zilizopo mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni, Mdee alitamka maneno dhidi ya Rais John Magufuli kuwa, ‘anaongea hovyo, anatakiwa afungwe breki,’ kitendo kinachodaiwa kuwa ni kumdhalilisha Rais na kusababisha uvunjifu wa amani.