Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 5:34 am

NEWS: KESI YA MBOWE YAPIGWA TENA KALENDA, ARUDI SEGEREA

Kesi Nambari 112/2018 inayowakabili Viongozi Wakuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe na Wabunge 7 wa Chama hicho imeendelea patupu leo asubuhi, Alhamis, Januari 31, kwa kutajwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam.

Kesi hiyo imepangiwa Hakimu mpya Kelvin Mhina, baada ya aliyekuwa hakimu anaye sikiliza kesi hiyo kupandishwa hadhi ya Ujaji katika mahakama kuu na imeaihirishwa hadi Februari 14/2019. na watuhumiwa Freeman Mbowe na Esther Matico wamerudishwa Mahabusu Segerea

Mbowe na Matiko wako gereza la Segerea baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana Novemba 23, 2018 kwa kukiuka masharti ya dhamana ikiwemo kutoka nje ya nchi bila kibali

Washitakiwa wengine kwenye kesi hiyo ya jinai namba 112/2018 ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicenti Mashinji; makatibu naibu wakuu, Salum Mwalimu (Zanzibar) na John Mnyika (Bara).

Wengine ni mbunge wa Kawe, Halima Mdee; mbunge wa Bunda, Mchungaji Peter Msigwa; mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.

Mbowe na viongozi wengine wanakabiliwa na mashtaka 13 ya uchochezi, uasi na kuhamasisha wafuasi wao kutenda makosa, hakuweza kufika mahakamani wakati kesi yao ilipotajwa.