Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 2:41 pm

NEWS: KESI YA MADAWA YA KULEVYA YAMPELEKA MTU MIAKA 20 JELA

Dar es salaam: Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, imemhukumu Tabia Omari kwenda jela miaka 20 na kulipa faini ya Sh 134 milioni , kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroine.

Tabia nimkazi wa Tandale Shuleni Maguniani, Jijini Dar es Salaam lakini ni mwenyeji wa Mkoa wa Morogoro , alihukumiwa kifungo hicho jana ( Ijumaa) na Jaji wa Mahakama Kuu Wilfrida Korosso.

Tabia alikamatwa Novemba11,2012 katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere akiwa na hati ya kusafiria namba AB 527070 iliyotolewa June 22,2012 alikuwa asafiri na Shirika la Ndege la Ethiopia kuelekea Hong Kong.

Baada ya kufanyiwa ukaguzi alikutwa akiwa amemeza vifungashio kama pipi 75 sawa na gram 994.47 za dawa za kulevya aina ya Heroine.

Jaji aliyetoa hukumu Wilfrida Korosso amesema ametoa adhabu hiyo baada ya kujiridhisha pasipo shaka kwamba mshtakiwa huyo alitenda kosa la kusafirisha dawa za kulevya.

Kwa upande wao Mawakili wa Serikali walioendesha kesi hiyo Mtalemwa Kishenyiri ambaye ni Wakili wa Serikali Mwandamizi na Clara Chalweni Wakili wa Serikali.

Waliiomba Mahakama kutoa adhabu kali ili iwefundisho kwa wale wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya iliwatambue kwamba yeyote anayepatikana na hatia sheria itachukua mkondo wake.