Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 7:15 am

NEWS: KESI YA LISSU DHIDI YA NDUGAI KUFUNGULIWA HIVI KARIBUNI

Mchakato wa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu, kumfungulia mashitaka Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, kufuatia uamuzi wake wa kumvua ubunge wa Singida Mashariki kiholela inaelezwa kwa sasa umekamilika.

Related image

Taarifa zilizotolewa leo Ijumaa Julai 19, 2019 na Rais huyo wa zamani wa TLS wakati akiongea na 'Mwanahalisi' amesema kuwa taratibu zote za kufungua shauri hilo zimekamilika; na kesi kamili yaweza kufunguliwa muda wowote wiki ijayo.

“Kwa kiasi kikubwa, taratibu zote za kufungua kesi hii zimekamilika. Kilichobakia kwa sasa, ni kwa mawakili wangu kumalizia malizia kupitia nyaraka zote zinazohitajika, ili tukiende mahakamani tuende tukiwa tumejiandaa vya kutosha,” anaeeleza. Lissu anasema, aliamua kukaa kimya kwa muda mrefu kutokana na kujiandaa na suala hilo na kwamba hakutaka kwenda mahakamani bila kukamilisha kwa taratibu zinazotakiwa.

Hapo awali taarifa ziliripoti kuwa kesi hiyo imekwama kufunguliwa mapema kufuatia kutokamilika kwa nyaraka muhimu, ikiwamo kukosekana kwa barua ya kumvua ubunge iliyoandikwa na Spika Ndugai kwenda Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Ndugai alitangaza kumvua ubunge Lissu, tarehe 28 Juni mwaka huu, kwa maelezo kuwa mwanasiasa huyo wa upinzani hafahamiki mahali aliko.

Aidha, Ndugai alidai kuwa Lisuu amevuliwa ubunge kwa sababu ya kushindwa kuwasilisha kwenye Tume ya Maadili ya Viongozi wa umma, taarifa za mali zake. Kwa muda wa takribani miaka miwili sasa, Lissu yuko nje ya nchi kwa matibabu, kufuatia kushambuliwa kwa risasi na wanaoitwa na serikali, “watu wasiofahamika.” Yafuatayo ni maelezo kamili ya Tundu Lissu, aliyoyatuma kwa MwanaHALISI na baadaye kusambazwa kwenye mitandao kadhaa ya kijamii.

"Kuna ambao wanalialia na kukata tamaa kwa sababu ya haya ya leo.

Hawa nawaambia mapambano haya yanahitaji akili, sio jazba na hasira. Wengi hawaelewi kinachoendelea, wanafikiri haya ya leo ndio mwisho wa safari yetu. Hawa ndio ninahitaji kuwafafanulia kinachoendelea. Kwanza, msichanganye ratiba ya Tume ya Uchaguzi na ratiba ya Mahakama Kuu. Ratiba ya Tume imekamilika leo. Wanachokiita uchaguzi kimefanyika. Kazi yao imekwisha. "

Ratiba ya Mahakama inaanza muda wowote kuanzia tarehe 29 Juni hadi 28 Desemba 2019. Maana yake ni kwamba ninaweza kufungua kesi katika siku yoyote ndani ya hicho kipindi cha miezi sita.

Hadi sasa hazijafika wiki tatu tangu uamuzi wa Spika Ndugai. Bado nina miezi mitano na wiki moja ya kufungua kesi. Kwa hiyo wanaolialia kwamba nimeachia ngazi, etc., wajue sijachelewa hata kidogo. Pili, mwenye haki ya kufungua kesi hiyo ni mimi mwenyewe au mwakilishi wangu ambaye nimempatia mamlaka ya maandishi ya kushtaki kwa niaba, yaani power of attorney.

Power of Attorney inatakiwa kusainiwa na mimi mwenyewe mbele ya kamishna wa viapo anayetambuliwa na sheria za Tanzania, basically wakili anayefanya kazi Tanzania anatakiwa kuja kunishuhudia sahihi huku niliko. Tatu, baada ya kusainiwa mbele ya kamishna wa viapo, power of attorney hiyo inatakiwa kusainiwa na huyo niliyemkabidhi mamlaka ya kuniwakilisha mahakamani, na saini yake hiyo ishuhudiwe pia na kamishna wa viapo. Nne, baada ya kusainiwa na wahusika wote, power of attorney hiyo inatakiwa kusajiliwa kwenye Ofisi ya Msajili wa Nyaraka Dodoma, Dar, Moshi au Mbeya na kulipiwa ushuru unaotakiwa." amesema Lissu