Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 9:43 am

NEWS: KESI YA LEMA YASUSIWA MAHAKAMANI

Dar es salaam: Kesi ya Kumkashfu Rais inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema imesuswa mahakamani baada ya wakili Sheck Mfinanga anayemuwakilisha Lema kwenye kesi hiyo kujitoa,Wakili Mfinanga alijitoa jana kuendelea na kesi hiyo kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa shauri hilo.

Sababu za kujitoa kwa wakili Mfinanga inakuja ikiwa ni miezi mitatu baada ya Hakimu Kisinda aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo, kujitoa kutokana na kuwekewa pingamizi na Jamhuri kuwa ana urafiki na mke wa Lema, Neema Lema

Mfinanga ametoa Sababu kuwa ni kutokana na upande wa utetezi kutopewa jalada la mwenendo wa kesi licha ya kuliomba mara tatu mahakamani hapo.

"Kwa sababu nimeshaleta notisi ya kukata rufaa naomba kuingia kwenye rekodi najitoa kuendelea kumwakilisha mteja wangu kutokana na ninachokiona kisheria kwamba tumeomba proceedings (mwenendo) na imeshindikana, mimi siyo wakili wake tena nimejitoa,” aliiambia mahakama jana

Kwa upande wake Lema aliishitumu mahakama na kusema kuwa hana imani na mahakama hiyo baada ya kesi yake hiyo kufungamana na kujitoa kwa wakili wake, na mahakimu. imemlazimu lema kuomba apewe muda zaidi wa kutafuta wakili mwingine na mahakama ikamkubalia na kuhairisha kesi hiyo mpaka Novemba 14 mwaka huu itakapo sikilizwa tena.