- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KESI YA KUBENEA KUNGURUMA SEPTEMBA 4
DODOMA: MAHAKAMA ya Wilaya ya Dodoma imeendelea kupiga kalenda kesi ya Mbunge wa Ubungo,Saed Kubenea kutokana na uchunguzi wa kesi hiyo kutokamilika,ambapo imeahirishwa hadi Septemba 4 mwaka huu.
Wakili wa serikali Foibe MagiliI, leo ameieleza Mahakama hiyo kuwa uchunguzi haujakamilika na hivyo kumuomba Hakimu James Kareyemaha kuiahirisha kesi hiyo hadi uchunguzi utakapokamilika.
Kufuatia ombi hilo la wakili wa Serikali kutaka kesi iahirishwe,Hakimu anayoiendesha kesi hiyo James Karayemaha aliliridhia ombi hilo ambapo aliaharisha kesi hiyo hadi Septemba 4 Mwaka huu.
Mshitakiwa kubenea anakabiliwa na kosa la kumshambulia Mbunge wa Viti maalum,CCM Juliana Shonza.
Hata hivyo Kubenea leo ameshindwa kufika Mahakamani kutokana na kudaiwa kufiwa na ndugu yake hivyo kulazimika kwenda msibani Mafia.
Aidha mshitakiwa huyo anatetewa na jopo la Mawakili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Mshtakiwa Kubenea anadaiwa kutenda kosa hilo mnamo Juali 3 mwaka huu katika eneo la Bunge Mjini Dodoma.
KUBENEA anakabiliwa na kesi ya shambulio kinyume cha Sheria kifungu namba 240 cha sheria ya makosa ya jinai sura ya 16 kilichofanyiwa marejeo mwaka 2002.