- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KESI YA KUBENEA KUJULIKANA KESHO
DODOMA: Kesi ya mbunge wa Ubunge, Saed Kubenea (Chadema) hatima yake itajulikana leo kama itahailishwa tena, kufutwa au kuendelea kusikilizwa.
Hali hiyo inatokana na Mahakama ya Wilaya ya Dodoma kuipiga Kalenda kesi hiyo hadi kesho 5 ambapo itatajwa.
Kwa mujibu wa Hakimu James Karayemaha amesema kesi inayomkabili Kubenea itatajwa (kesho) leo baada ya wakili wa serikali, Lina Magoma, kueleza kuwa kuna mambo mbalimbali ambayo yana upungufu katika jarada la kesi ambayo inamkabili mbunge huyo.
Awali kabla hakimu Karayemaha kutaja siku ya kutajwa kwa kesi ya Kubenea,wakili wa serikali amemuomba Hakimu pamoja na wakili wa Kubenea,Kuwayawaya Sitivine Kuwayawaya,alimuomba mshitakiwa pamoja na baadhi ya wale waliokuwa wakisikiliza kesi watoke nje kwanza ili watete kutokana na kile ambacho wakili wa serikali kudai kuwa faili lilikuwa linamarekebisho kidogo.
Kubenea anashtakiwa kwa kosa la jinai ambalo anadaiwa kumshambulia mbunge wa viti maalum (CCM), Juliana Shonza wakati wa bunge la bajeti.
Hakimu James Karayemaha alipanga tarehe hiyo na wakili wa serikali, Lina Magoma, alikubaliana naye hivyo kesi hiyo itaendelea Septemba 5, mwaka huu.
Awali Kubenea alisema utaratibu wa kisheria uliotumika siyo mzuri hivyo ni vyema kesi hiyo ingebaki polisi hadi hapo upepelezi utakapokamilika na kwamba ni matumizi mabaya ya rasilmali za serikali.